Visa vya ukeketaji vyazidi kuongezeka katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa nchi
7th February, 2016
Visa vya ukeketaji miongoni mwa jamii nchini Kenya,vimetajwa kushuka kwa kiasi ulimwengu kote ingawa humu nchini kuna baadhi ya jamii zinaendeleza unyama huo kwa mtoto wa kike. Sehemu ya kaskazini mashariki ya Kenya,jamii ya wasomali inaongoza kwa kuendeleza visa vya ukeketaji kwa asilimia 94. Hivi maajuzi nilijionea juhudi za kupunguza ukeketaji miongoni mwa jamii,huku dada mmoja akijutia kukeketwa baada ya madhara yake kumuathiri hadi leo katika kata ya Arbaqaramso,kaunti ya Wajir. Tazama taarifa yenyewe niliokuandalia wakati ulimwengu ukisherehekea siku ya kimataifa kupinga ukeketaji hapo jana.