Kaunti ya Samburu yakabiliana na visa vya ukeketaji wa watoto wa kike
16th December, 2015
Kaunti ya Samburu imekuwa ikikabiliana na visa vya ukeketaji wa watoto wa kike ambao ni kunyume na sheria za Kenya….ripoti zimebaini kuwa asilimia 96 ya wasichana katika eneo hilo huathiriwa na tamaduni hizi huku wengine wakiripotiwa kuolewa mapema. Kutokana na hayo, wasichana wa makao ya Consolata wameridhia kutosherekea sikukuu za Krismasi na wapendwa wao na badala yake kusalia kwenye makao hayo kutokana na hofu kuwa masomo yao yatakatizwa na ndoa za mapema au hata ukeketaji, viloshika kasi msimu huu