×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Wabunge watatu wa CORD wametimuliwa bungeni kwa kigezo cha utovu wa nidhamu

18th February, 2015

Wabunge watatu kutoka CORD wametimuliwa kwa muda kutoka bungeni kwa kigezo cha utovu wa nidhamu.John Mbadi ambaye ni mbunge wa Suba, Silverse Anami mbunge wa Shinyalu na Gladys Wanga ambaye ni mbunge wa kaunti ya Homa Bay wametimuliwa kupitia uamuzi wa kura uliofanywa bungeni. Wabunge hao watatu wanatuhumiwa kwa kushiriki kwenye vurugu iliyoshuhudiwa bungeni mwezi disemba mwaka uliopita wakati wa mjadala kuhusu mabadiliko kwenye sheria ya usalama.wabunge 101 waliokuwa bungeni waliunga mkono kutimuliwa kwa watatu hao, wabunge 52 walipinga na wawili kususia kura hiyo.watatu hao hawataruhusiwa kushiriki vikao vya bunge kwa muda wa siku nne.wabunge kutoka CORD wanamtaka spika wa bunge pia kuwatimua wabunge watano kutoka Jubilee ambao pia wanadaiwa kushiriki kwenye vurugu hilo.
.
RELATED VIDEOS