Tume ya Uwiano na Utangamano yaanza kazi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya
2nd October, 2014
Kamati maalum chini ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa iliyopewa jukumu la kutatua mizozo ya eneo la kaskazini mashariki mwa kenya imeanza kutekeleza majukumu yake. Hii leo mwenyekiti wa tume hiyo na aliyekuwa spika wa bunge francis ole kaparo alifanya majadiliano ya kuleta amani kati ya jamii ya gare na degodia. Kwa kauli moja viongozi wa jamii hizo mbili walikubaliana kukomesha mapigano. Kamati hiyo sasa itatembelea eneo hilo ili kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na vita hivyo, huu ukiwa ni mkutano wa pili kwa kamati hiyo katika hali ya kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya makabiliano ya mara kwa mara kati ya jamii hizi.