x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Timu zitakazo shiriki Copa Coca Cola yajua vikundi vyao leo

05, Aug 2014

Mabingwa watetezi wa kombe la Copa Coca Cola, chuo cha JMJ hapa jijini Nairobi wamewekwa kundi moja na Murhanda Youth kutoka magharibi mwa Kenya katika mashindano ya mwaka huu. Timu zingine kwenye kundi b ni shule ya wavulana ya tana na shule ya angaza. Chuo cha jmj kilifuzu kwa fainali ya mwaka huu baada ya kuwabandua nje makadara juniors katika eneo la Nairobi. Mechi za mwaka huu zitachezwa katika uwanja wa Hope Centre ulioko eneo la Kawangware. Lakini mechi za fainali zitachezwa katika uga wa City. Timu ya Kisumu Lakers ambao walipoteza kwenye fainali ya mwaka jana wako kundi a pamoja na Kitale Youth, Young Muslims, na Tharaka stars. Katika droo iliondaliwa leo katika makao makuu ya kampuni ya Coca Cola hapa jijini, timu mbili kutoka Nairobi, Beijing raiders na Kibra Queens ziliwekwa kwenye kundi A. Shule ya Shinyalu, na Cherangani Starlets wako kundi hilo pia.

RELATED VIDEOS


Feedback