Hali ya njaa na ukame yazidi kuwa mbaya zaidi Turkana
29th January, 2014
Wakati hifadhi kuu ya visima vya maji ya kiwango kikubwa chini ya ardhi vilipogunduliwa mwaka jana, serikali ya Kenya ilitangaza kuwa hifadhi hio ya maji ina uwezo wa kumudu mahitaji ya maji katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini ijayo kote nchini. Lakini miezi chache baadaye, visa vya kusikitisha vya wakenya kuchinja na kula nyama ya mbwa kutokana na njaa vimeripotiwa eneo hilo la Turkana. Je serikali imesahau majukumu yake muhimu ya kuleta maendleo humu nchini, na badala yake kuzingatia sana siasa?