×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Kijana wa Dandora amkabidhi Sonko bunduki

20th September, 2013

Kijana mmoja wa Dandora leo aliitikia mwito wa seneta wa Nairobi Mike Sonko, kwa kusalimisha bunduki aina ya Ak47. Na papo hapo akatunukiwa shilingi elfu hamsini. Juzi akiwa dandora, Sonko alitoa ahadi kwa vijana kuasi uhalifu, na kusalimisha silaha haramu. Katika kituo cha polisi cha Baba Dogo, Joram Magero ama kwa jina lingine Oscar alifika akiandamana na mkewe na kupeana bunduki iliokuwa imefungwa na karatasi za plastiki. Waliokuwepo katika shughuli hii ilikuwa ni pamoja na mkuu wa polisi wa Nairobi, Benson Kibue. Sonko alisema aliamua kufuata mkondo huu kama harakati za kupunguza visa vya uhalifu hapa jijini. Lakini ni Joram ndie aliyewashangaza wengi pale alipoangua kilio alipokuwa akisalimisha bunduki hiyo. Alisimulia jinsi anavyoishi kwa hofu, kwa kuwa inadaiwa yeye ni mhalifu sugu na anasakwa kwa udi na uvumba. Kibue alimhakikishia Joram na wengine watakaofuata nyayo zake kwamba hawatadhuriwa na yeyote.
.
RELATED VIDEOS