21st March, 2022
Jamaa mmoja mwenye asili ya Sudan kusini ameaga dunia huku wenzake wanne wakijeruhiwa baada ya kushambuliwa na raia nyumbani kwao mawanga, Nakuru. Katika kisa kilichozua kiwewe baina ya wakenya na wasudan kusini wanaoishi nakuru, kundi la watu linadaiwa kuvamia nyumba walimokuwa wakiishi raia sita wa sudan kusini na kuiteketeza kwa madai kuwa walikuwa wamemnyanyasa mwanamke mmoja. polisi wamesalia kimya kuhusu kisa hicho huku ubalozi wa sudan kusini ukitaka waliotekeleza kisa hicho kukamatwa. ibrahim karanja anaarifu.