14th March, 2022
Taarifa kinzani zimeibuka leo kuhusu alichotia saini kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, katika mkataba wa makubaliano kati yake na muugano wa Azimio, uliomuidhinisha kinara wa ODM Raila Odinga kupeperusha bendera ya Azimio katika uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Katika mahojiano ya kipekee na runinga ya Ktn News, Kalonzo alisema alikubaliana kuunda muungano mwingine mkubwa wa Azimio?Oka, kinyume na walivyoeleza wasemaji wa Raila leo.
Licha ya kukaribisha ushirikiano na Kalonzo, upande wa mawasiliano katika muungano wa Azimio ulishikilia kwamba habari za kalonzo hazikuwa sahihi.