.
14th March, 2022
Waziri wa elimu Prof. George Magoha ameonya dhidi ya walimu na wanafunzi kujihusisha katika udanganyifu wa mtihani wa kidato cha nne KCSE ambao umeanza hii leo kote nchini.
Waziri Magoha, alisimamia shughuli ya usambazaji wa mitihani hiyo katika kaunti ya Mombasa huku viongozi kadha wa kadha serikalini wakikagua shughuli hiyo katika sehemu mbalimbali nchini.