×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Zilizala La Westgate na Mohammed Ali

18th October, 2013

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, zimekuwa siku nyingi za kubashiri, na siku nyingi za kunongonezana kuhusu kilichojiri wakati taifa lilitekwa nyara na magaidi kwa siku nne mtawalia. Wakenya zaidi ya sitini walipoteza maisha yao katika jumba la Westgate lakini hadi sasa Wakenya hawajajua ukweli kuhusu yaliyojiri katika jumba la Westgate. Je ni kweli kuna waliokuwa wametekwa nyara na magaidi na kuzuiliwa katika jumba hilo? Je ni kweli kuna magaidi waliouawa na wanajeshi? Meza ya upekuzi ya Jicho Pevu na Inside Story usiku na mchana wamekuwa wakidurusu kila ukurasa na, kufanya mahojiano na kupitia hatua kwa hatua video za cctv kutoka jumba la Westgate na sasa wako tayari kukusimulia kilichojiri bila kuficha lolote. Meza hii ilifanikiwa picha za pekee kuhusu matukio ya Westgate. Usiambiwe tena tizama makala haya yatakayokujia katika muda usiokuwa mrefu ukiwanaye mwanahabari mpekuzi mohammed ali.
.
RELATED VIDEOS