Mlinda lango wa timu ya mpira ya magongo Cynthia Akinyi atuzwa mwanamichezo bora wa mwezi wa Januari

Sports | Wednesday 14 Feb 2018 7:57 pm

Mlinda lango wa timu ya mpira wa magongo ya Telkom Cynthia Akinyi ametuzwa mwanamichezo bora wa mwezi Januari. Cynthia ambaye ni mchezaji wa saba kupokea tuzo hiyo amewapiku wachezaji tenisi Ryan Randiek na Sneha Kotecha pamoja na mwanabondia Nick Okoth, mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 24 alikuwa nguzo muhimu katika kampeni ya Telkom kwenye mashindano ya klabu bingwa afrika ambapo alifungwa mabao amwili pekee kuwasaidia kumaliza kwenye nafasi ya pili.