.
8th December, 2021
Wachimba migodi watatu waliokuwa wamekwama katika mgodi wa dhahabu eneo la Bondo kaunti ya Siaya wameokolewa.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi eneo la Bondo wachimba migodi hao wameondoleewa katika mgodi huo majira ya saa nane alasiri leo.
Watatu hao wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ndogo ya kaunti huko Bondo. Hii imefikisha idadi ya wachimba migodi hadi saba waliokolewa wakiwa hai kutoka mgodi huo kuporomoka.