.
27th February, 2021
Serikali ya kaunti ya Mombasa imefunga maeneo ya kutupa taka ambayo hayakuwa yameidhinishwa katika maeneo tofauti kaunti hiyo ili kuhakikisha mazingira safi katika kaunti hiyo. Wenyeji wa kaunti hiyo wamehimizwa kuzingatia kutotupa taka ovyo ili kudumisha hali ya usafi. Kitengo cha mazingira na kawi kimeanzisha zoezi la kusafisha mji huo ambapo wakazi wa Changamwe, Nyali, Mvita, Likoni, Jomvu na Kisauni wamehimizwa kuhakikisha mazingira yao ni nadhifu