.
27th February, 2021
Wakulima wa mahindi eneo la north rift wanapinga hatua ya bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB kupunguza bei ya mahindi kutoka shilingi 2700 hadi shilingi 2550 kwa gunia la kilo tisini. Wakulima waliowasilisha mahindi yao katika maghala yaliyoko Eldoret walishangaa baada ya kubaini kwamba bei ya kila gunia la kilo tisini imepunguzwa kwa shilingi 150. Wakulima hao wanadai kwamba, bei hiyo ilibadilishwa bila ilani kutolewa