Muthama na Murkomen watofautiana kuhusu pendekezo la kumleta Kalonzo katika chama cha UDA
26, Jan 2021
Wanasiasa wa chama cha U.D.A wametofautiana kuhusu pendekezo la kumleta chamani kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka. Walikuwa katika kaunti ya Machakos walikopeleka kampeni za kiti cha useneta. Waligawanyika kimawazo, upande mmoja ukisema Kalonzo asiachwe nje kwenye mipangilio yao, huku wapo walidai kwamba Kalonzo hana nafasi kwenye siasa za mrengo wao.