.
25th January, 2021
Watu kumi na wawili, tisa miongoni mwao wakiwa wakenya wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mandera kufuatia mapigano ya vikosi vya kijeshi kutoka taifa la somalia na jubaland.
Kenya sasa imeiandikia tume ya umoja wa Afrika ( AUC) kuelezea wasiwasi wake kuhusu hali hiyo kwani huenda ikazua janga la kibinadamu iwapo hatua hazitachukuliwa mapema.
Taifa la somalia limekuwa likishutumu kenya kwa madai ya kuliyumbisha kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi ujao lakini serikali ya kenya kupitia waziri wa usalama wa ndani Dr. Fred matiang’i imekanusha madai hayo na kushikilia kuwa kinachoshuhudiwa ni masuala ya ndani ya Somalia.