.
4th December, 2020
Kiongozi wa chama cha odm raila odinga amesema muda wa kupokea maoni zaidi kuhusu mswada wa kurekebisha katiba umekwisha na kilichopo sasa ni kwa wakenya kujiandaa kwa kura ya maamuzi. Raila, amepinga vikali wito unaosukumwa na mrengo wa naibu rais william ruto kwamba kura ya maamuzi iandaliwe kwa wakati mmoja na uchaguzi mkuu wa 2022. Raila na kundi la wanasiasa wanaomuunga mkono, pia walipuzilia mbali pendekezo la naibu rais William Ruto kwamba mswada huo ugawanywe kwenye vipengele kadha kabla kura ya maamuzi ili kuzuia kuigawanya nchi kati ya wanaounga au kupinga mswada huo