18th September, 2020
Watu wengine wanne wamefariki katika muda wa saa 24 zilizopita kutokana na makali ya virusi vya korona huku maambukizi mapya 148 yakirekodiwa hii leo. idadi ya vifo sasa ni watu 646 na maambukizi 36, 724.miongoni mwa walioambukizwa 145 ni wakenya na watatu ni raia wa kigeni.umri wa waathiriwa ni kati ya miaka 2 na 75.kaunti ya mombasa ndio imerekodi visa vingi ikifuatwa na nairobi.kaunti nyengine ambazo zimeandikisha maambukizi mapya ni laikipia, kiambu, nakuru,embu, uasin gishu, kajiado, taita taveta, kisumu. Kitui, trans nzoia, baringo, elgeyo marakwet, kwale, machakos, kericho, makueni na muranga.habari njema ni kuwa watu wengine 98 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona hadi watu 23,709.