.
24th January, 2022
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi COTU Francis Atwoli amemjibu vikali kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi kuhusiana na matamshi yake ya hapo jana ambapo alimshambulia Atwoli na COTU kwa madai ya ubadhirifu wa fedha za wafanyakazi.
Atwoli amemtaja Mudavadi kama mwanasiasa asiyekuwa na uhakika na mwenye hofu ambaye haelewi jinsi vyama vya kutetea maslahi ya wafanyikazi huendesha maswala yake.