7th February, 2021
Je, mtoto wako wa kiume yu salama kiasi gani katika shule ya bweni, achezapo nyumbani ama aendapo dukani ? Imebainika kuwa wanaume wengi wameishi na sonono na kiwewe cha kulawitiwa wakiwa shuleni ama wakicheza mitaani. Wengi wamekuwa hadi kuja kuoa sasa wanaitwa baba, ila athari za kisaikolojia wanaishi nazo na kujiona kuwa si wananume kamili kwa vitendo walivyofanyiwa wakiwa wadogo. Je, taasisi za kuwafanya wanaume wafunguke na kuelezea madhila ya ubakaji na ulawiti bila unyanyapaa zipo? Majibu na maswali zaidi yako kwenye simulizi za wavulana na wanaume, Kwenye makala ya nyuzi za ulawiti na mwanahabari wetu Lofty Matambo ?