18th June, 2021
Asasi zote za serikali zimetoa hakikisho la kumuunga mkono jaji mkuu Martha Koome anapohudumu kwenye wadhifa wa jaji mkuu. spika wa bunge la seneti, waziri wa ulinzi Monica Juma na viongozi wengine vile vile wamempongeza Martha Koome ambaye pia ni jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini. Wamesema hayo kwenye hafla ya kumpongeza Martha Koome, iliyoandaliwa hapa jijini Nairobi na kuhudhuriwa na wakuu wengine serikalini, wadau wa tume za kitaifa na idara ya mahakama.