5th June, 2020
Kenya imerekodi visa 134 vipya kwa muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha visa vyote nchini hadi 2474. Kaunti za Mombasa,Nairobi na Busia,zimeendelea kusajili idadi za juu mfululizo ya visa vya maambukizi ya virusi vya korona. Visa hivi sasa vikitarajiwa kuchangia namna serikali itakavyotoa mwelekeo hapo kesho wakati ambapo muda wa kafyu ya macheo hadi machweo ikitarajiwa kufikia ukingoni.