29th May, 2020
Viongozi kutoka magharibi mwa kenya wamekutana nyumbani kwake katibu mkuu wa vyama vya wafanyikazi nchini Francis Atwoli na kuazimia kufanya kazi pamoja kiuchumi na kisiasa. Wanasiasa kutoka katika mirengo yote ya siasa walihudhuria hafla hiyo na baadhi ya maazimo ni pamoja na kuwateua katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli, gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na Spika wa bunge la senate Kenneth Lusaka na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa kuelekeza jamii hiyo kuhusu mielekeo ya siasa miongoni mwa mambo mengine. Kadhalika waliwateua viongozi watakaofuatilia maswala ya eneo la magharibi katika bunge la kitaifa na lile la senate