Klabu ya AFC Leopard yazindua ufadhili rasmi na kampuni ya Sportpesa
2nd March, 2016
Klabu ya AFC Leopards imezindua rasmi ufadhili wa kampuni ya sportpesa utakaoendelea kwa muda wa miaka mitano. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli moja hapa jijini nairobi unatazamiwa kuirejesha klabu hiyo katika hadhi yake ya zamani. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wasimamizi wa ingwe, washikadau wa kandanda nchini na pia wachezaji wa zamani wa AFC Leopards ambao wana imani kuwa ufadhili huo utasaidia pa kubwa katika kampeni yao ya kunyakua taji la ligi kuu nchini msimu huu.