Watu watano wamekamatwa na 46 kujeruhiwa baada ya waandamanaji wanaotaka uhuru wa jimbo la Catalonia kuwarushia mawe maafisa wa polisi wakati wa pambano la El Clasico baina ya Barcelona na Real Madrid ambalo awali lilikuwa limeahirishwa kwa hofu za kiusalama.
Watu kadhaa walijeruhiwa waandamaji walipokabiliana vikali na polisi karibu na uga wa Nou Camp mechi hio ikiendelea.