Hivi karibuni, jumuia ya Afrika Mashariki ilimteua Rais Yoweri Museveni kuwa mpatanishi mkuu kati ya serekali ya Pierre Nkurunziza na mahasimu wake. Hali tete Burundi ilizoroteka zaidi wakati mwasi mmoja mkuu bwana Godefroid Niyombere, alisema katika mahojiano na stesheni ya KTN kwamba wakosoaji wa serekali ya Nkurunziza wameamua ni vita pekee vitakavyo weza kutatua mbarika ya kisiasa Burundi.
Changamoto zilizoikumba Burundi zilidhihirika wazi wakati bwana Nkurunziza alipowania hatamu ya tatu kwenye uchaguzi wa urais. Jumuia ya Afrika Mashariki iliyokutana Dar es Salam jumatatu wiki hii ilipendekeza kuahirisha uchaguzi wa rais kwa wiki mbili kutoka July 15th hadi July 30th 2015.