Huku hamahama za chama zikizidi kupamba moto miongoni mwa “viongozi watarajiwa” sehemu mbalimbali nchini, wagombea wamekuwa wakikesha usiku kucha na kuweka mikakati thabiti zitakazo hakikisha wanawania na kuibuka washindi katika viti kadhaa serikalini. Majuma kadhaa yaliyopita, tulimshuhudia aliyekuwa seneta wa Kakamega Bonny Khalwale akikigura chama cha Ford Kenya na kutangaza hadharani kumuunga mkono naibu rais William Ruto katika azimio lake la kuwania urais kwa uchaguzi mkuu ujao.