Ni nadra sana kuzipata habari njema za michezo, hasa soka, kutoka nchini Kenya. Hii ikichangiwa pakubwa na hatua ya aliyekuwa Waziri wa Michezo Dr. Amina Mohamed kuvunjilia mbali lililokuwa shirikisho la soka nchini FKF.
Kuvujiliwa mbali kwa FKF, kuliandamwa na kufungiwa nje kwa soka la Kenya na shirikisho la soka duniani, FIFA. Kwa maana hii ni kuwa mama Amina aliachia 'uongozi' wa soka mikononi mwa kamati simamizi/kamati andalizi na kila aina ya kamati. Matokeo yake je? Marufuku yakawa kwa miezi tisa!