Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Bahari na Uvuvi, KEMFRI imekuwa ya hivi punde kuipongeza hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku utumiaji wa chupa za plastiki katika mbuga za kitaifa, misitu na kwenye fuo za bahari kuanzia tarehe tano mwezi Juni mwaka ujao.
Meneja wa tasisi hiyo, Erick Ochieng amesema hatua hiyo itakabili athari kwa wanyama wa baharini ambayo imekuwa ikisababishwa na utupaji ovyo wa taka za plastiki.