Kikwetu - kikuyu culture - swahili
Dhana mbalimbali hukabili jamii nyingi za humu nchini na kukita mizizi kuhusiana na kundi husika. Kuna watu au jamii zinazodhaniwa kuwa watu wakaidi, wenye hasira,wenye tamaa ya pesa,na hata kuwa wavivu. Jamii ya wakikuyu haijanusurika kutoka katika dhana hii kwani wengi wao hudhaniwa kuwa wapenda pesa na hata wenye uwezo wa kufanya lolote lile ili kupata pesa hizo hata kama ni kwa njia ya kuiba. Lakini wenyewe wanazipinga vikali dhana hizi kwa kusema kuwa wao hutegemea jasho lao na bidii yao ndio inayowapatia motisha ya kujitafutia pesa.
Share this story