Mahasibu watakiwa kukabili ufisadi

News
By Sam Amani | May 24, 2022

Waziri wa Usalama na Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiang'i amewataka mahasibu kuwa mstari wa mbele kukabili ufisadi katika sekta ya umma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku tatu la Mahasibu jijini Mombasa, Matiang'i amedokeza kwamba kesi zote za ufisadi katika taasisi mbalimbali za serikali zimechangiwa na mahasibu ambao wamekuwa wakizindisha kiasi cha fedha zinazohitajika kutekeleza miradi mbalimbali vilevile kutoa huduma kwa umma.

Matiang'i ametoa mfano wa ripoti moja iliyolenga kutathmini matumizi ya fedha katika Idara ya Magereza ambapo matumizi yake yalizidishwa na kufikia takribani shilingi bilioni 6.

Aidha, ameeleza haja ya mahasibu kutunza rasilimali za umma, kuhakikisha zinatumika ipasavyo ili kuepusha hali ya matumizi mabaya ya fedha.

Kongamano hilo linalenga kujadili mbinu za kufufua uchumi hasa kufuatia athari za janga la korona.

Share this story
Kirimi powers to glory at VetLab Club event
Ericv Karimi is the overall winner of the eighth and final leg of the Kengen golf tournament series. 
Strathmore Swords bounce back to slice Eldonets in league battle
Strathmore University Swords bounced back from Saturday’s defeat to edge out Eldonets 67-64 in a Kenya Basketball Federation (KBF) Women’s Premier League match on Sunday.
K'Ogalo silence Muranga Seal to move one win away from title
Record league champions Gor Mahia moved to within one win of another league title after beating Murang’a Seal 3-1 in a crucial SportPesa Premier League match on Sunday.
African stars in Europe: Antoine Semenyo wins it for City
Antoine Semenyo produced one of the great FA Cup final goals with an audacious back-flick that sealed a 1-0 win for Manchester City over Chelsea in the FA Cup final at the weekend.
Mixed results for top boxers as Police, KDF lead after first leg
Defending champions Kenya Police and Kenya Defence Forces shared the lead after the opening leg of the National Boxing League in Nakuru, as several top boxers suffered surprise defeats.
.
RECOMMENDED NEWS