Ruto atangaza timu ya watakaowania ubunge Nairobi

News
By Esther Kirong' | May 02, 2022

Mwaniaji wa urais wa Chama cha UDA william Ruto ametangaza orodha ya wagombea wa ubunge kwenye Kaunti ya Nairobi.

Katika orodha hiyo, Wakili Nelson Havi atawania Kiti cha Ubunge kwenye eneo la Westlands, John Kiarie atatetea kiti chake cha Dagoretti Kusini kwa tiketi ya UDA, Nixon Korir-Lang'ata huku aliyekuwa mchezaji wa kandanda wa Inter-Milan, McDonald Mariga akiwania ubunge Kibra kwa mara ya pili.

Billian Ojiwa atawania Mathare, Simon Mbugua wa EALA, Starehe, Rabow Hassan Kamukunji, Anthony Waithaka Makadara, George Theuri Embakasi Magharibi, Francis Muriithi akiwania Embakasi Mashariki, Mejja Donk Embakasi ya Kati na David Gakuya, Embakasi Kaskazini huku Ulbunus Kalumba akiwania Embakasi Kusini.

Ikumbukwe Chama cha Azimio la Umoja One Kenya kilitangaza orodha ya wagombea wake wa nyadhifa mbalimbali mwezi uliopita.

Mirengo ya Azimio na Kenya kwanza inayojumuisha UDA, inatarajiwa kuchuana huku kivumbi kikali kikitarajiwa kutifuliwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Share this story
Ronaldo, 41, leads Portugal into his sixth World Cup
Veteran Portugal striker Cristiano Ronaldo will lead his country into the 2026 World Cup this summer after coach Roberto Martinez named the 41-year-old in his squad on Tuesday.
Kenya's Afcon dream is under threat as FKF officials fight
FKF president Hussein Mohamed insists the National Executive Committee meeting of April 24, which voted to suspend him, was irregular, unconstitutional, and in his own words, a coup.
Kenyans now shift focus to Commonwealth Games after shining at Africa meet in Accra
After an overall second place in the continent at the 24th African Senior Athletics Championships, Kenyan stars have firmly set their sights on the Commonwealth Games in July.
New motorsports body up and running with autocross action at Stoni Athi
There was jubilation as fans welcomed the recognition of Motorsports Kenya Federation by the government as the official and legitimate motorsport governing body in the country.
Fight for survival now down to one team as Bidco, Sofapaka relegated
The battle to survive relegation in the SportPesa Premier League is set for a tense finish with five clubs still fighting to avoid joining Bidco United and Sofapaka in the National Super League.
.
RECOMMENDED NEWS