Polisi na waandamanaji wakabiliana wakati wa El Clasico [Picha]

Football
By Beldeen Waliaula na GameYetu | Dec 19, 2019
Watu kadhaa walijeruhiwa waandamaji walipokabiliana vikali na polisi karibu na uga wa Nou Camp [Courtesy]

Watu watano wamekamatwa na 46 kujeruhiwa baada ya waandamanaji wanaotaka uhuru wa jimbo la Catalonia kuwarushia mawe maafisa wa polisi wakati wa pambano la El Clasico baina ya Barcelona na Real Madrid ambalo awali lilikuwa limeahirishwa kwa hofu za kiusalama.

Watu kadhaa walijeruhiwa waandamaji walipokabiliana vikali na polisi karibu na uga wa Nou Camp mechi hio ikiendelea.

Waandamanaji hao walijifunika nyuso zao, waliasha moto barabarani na kuwatupia polisi mawe, ambao nao walijibu kwa kufyatua risasi katika barabara moja karibu na uga huo uliokuwa unaandaa mechi ya kwanza ya El Clasico ya msimu huu.

Watu watano walitiwa mbaroni na 46 kujeruhiwa katika maandamano hayo yanayonuia uhuru wa Catalonia. Kwa mujibu wa asasi za kutoa huduma za dharura, watu wanane walikimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Watu watano wamekamatwa [PICHA: TONI ALBIR/EPA-EFE/REX]

Waandamaji ambao wengi wao walibeba bendera za kushinikiza kujitenga kwa Catalonia, walifunga barabara na wakitumia vizuizi ambavyo walivitia moto polisi walipowasili ndani ya idadi kubwa ya magari.

Waandamanaji hao walivamia gari moja la polisi na kung'oa mabango yenye alama za barabarani na vilevile kuyaongeza katika vizuizi kwenye barabara.

Haya yalikuwa maandaamno ya kwanza ya kivita tangu Oktoba, ambapo mahakama kuu ya Uhispania iliwapokeza kifungo viongozi tisa wa kundi la kushinikiza uhuru wa Catalonia kwa mchango wao katika jaribio la uhuru la mwaka 2017 ambalo liliambulia patupu.

Mchuano huo wa jumatano ulikuwa umeratibiwa kuwepo mwezi oktoba lakini ukaahirishwa kutokana na sababu za kiusalama baada ya maandamano kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa kaskazini mashariki mwa Uhispania.

Waandamanaji hao walivamia gari moja la polisi na kung'oa mabango yenye alama za barabarani [PICHA:TONI ALBIR/EPA-EFE/REX]

Maandanamo hayo yalipangwa na kundi la kisiri linalolenga uhuru wa Catalonia. Lengo kuu la kundi hilo ni kushinikiza uhispania kushiriki mazungumzo ya kujitenga kwa jimbo hilo kando na kuachiliwa kwa raia wao walioshikwa wakipigania uhuru wa Catalonia.

Wakiimba 'uhuru' na 'achilieni wafungwa wa kisiasa', maelfu ya waandamananji wa Catalonia walikusanyika karibu na Nou Camp masaa machache kabla ya mechi hiyo iliyoambualia sare tasa.

Licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya polisi, waandamanji wengine walifunga moja ya barabara kuu karibu na uga huo na kusababisha msongamano wa magari kabla ya mechi.

Dakika chache kabla ya mechi, polisi walizima vita vilivyoibuka dhidi ya mashabiki wa barcelona na baadhi ya waandamanaji, na kutia mbaroni mtu mmoja kwa kuwatupia vifaa.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili, waandamanaji waliojifunika nyuso zao walibomoa ua wa nje lakini wakashindwa kuingia ndani ya Nou Camp, kwa mujibu wa msemaji wa polisi.

Kundi hilo liliwasha moto kwa mapipa ya takataka barabarani kabla ya magari ya polisi kuwasili na kuwatawanya, picha za shirika la REUTERS zinaonesha.

Waandamaji wengi walibeba mabango yenye maandishi "uhispania, keti tuzungumze" na kundi hilo la democratic tsunami, kupitia mtandao wa twitter, lilisema kuwa litasambaza laki moja ya mabango hayo kwa watu ambao wangehudhuria mechi hiyo.

Kundi hilo vilevile limewaambia watu kubeba mipira inayoweza kushika moto kirahisi na kuitumua "kuandikia dunia ujumbe".

Share this story
McKittrick and co crowned Rhino Charge champions
Rishi Chauhan of Team Pumba Patrol claimed victory in the newly introduced Half Charge category.
Sivanto Prime close in on Kinsman Cup title
Hussar made a comeback to defeat Redigo Deter 4.5-4.
Kenya Sevens promoted to World Rugby Sevens Series
Shujaa promoted after thrashing Germany 33-15 on Sunday.
SCHOOLS: Kisumu Day thrash Kisumu Boys 4-0 to qualify for Kisumu County finals
Both teams will be at Maseno School for the 2024 Kisumu County games set for June 12.
.
RECOMMENDED NEWS