Rais Mteule, William Ruto amewahakikishia Wakenya kwamba serikali yake itazingatia haki kwa kila mmoja na kudumisha demokrasia katika utendakazi wake bila mwingilio wa taasisi za serikali.

Akiwahutubia viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza mtaani Karen hapa Nairobi, Ruto amesisitiza kwamba serikali yake itazingatia sheria na kuheshimu katiba.

Katika kikao hicho, Ruto aidha amewahimiza viongozi hao kujiandaa vilivyo kutekeleza ahadi walizoweka wakati wa kampeni akisema wana jukumu kubwa la kufanikisha miradi ya maendeleo mashinani.

Wakati uo huo, Ruto amewaomba viongozi wote nchini kushirikiana na serikali yake, ili kuwahudumia Wakenya waliowachagua.

Vilevile Ruto amewahakikishia Wakenya kwamba serikali yake itawajibikia maslahi yao kwa hali yoyote ile. Katika kufanikisha hilo, Ruto amesema kupitia uongozi wa mabunge la Kitaifa na Seneti yatapitisha mswada unaolenga kuwashurutisha mawaziri kufika mbele ya bunge kujibu maswali kuhusu utendakazi wa wizara zao. Aidha, ameongeza kwamba serikali yake haitakubali watumishi wa umma kujihusisha na siasa.

Katika Muungano wa Kenya Kwanza mia moja sitini na watatu ambapo wa Chama cha UDA kina mia moja arubaini na maseneta ishirini na wanne. Aidha wabunge huru kumi miongoni mwa kumi na wawili waliochaguliwa majuzi vilevile wamejiunga na Kenya Kwanza.

.

Keep Reading


Ruto Senate Nairobi