Na, Beatrice Maganga Maraga awasihi wanasiasa kutoiingilia mahakama Jaji Mkuu, David Maraga ametoa wito kwa wanasiasa kujiepusha na mienendo yenye uwezo wa kuhitifaliana na utendakazi wa majaji. Katika kikao na wanahabari, Maraga ametoa mfano wa kisa ambapo Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Adan Duale alimkosoa hadharani jaji George Odunga kuhusu maamuzi mbalimbali ambayo amekuwa akifanya. Aidha amekitaja kisa cha Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto kudai kwamba upinzani ulikuwa ukishirikiana na mahakama kuhakikisha uchaguzi mkuu unaahirishwa kupitia kesi mbalimbali zilizowasilishwa mahakamani. Maraga aidha amesema kila jaji ana uhuru wa kufanya maamuzi katika kesi mbalimbali zilizo mbele yake bila shinikizo la aina yoyote. Aidha amesisitiza kwamba idara ya mahakama i tayari kuzishughulikia kesi mbalimbali zitakazowasilishwa mbele yake kuhusu uchaguzi mkuu.