Na, Hassan Ali

 Jarida la Sun ladai kuwa baada ya lalama nyingi kutoka kwa mashabiki, sasa kocha wa Arsenal Arsene wenger anapanga kuwasajili wachezaji Robert Lewandowski kutoka Bayern Munich, na labda Mfaransa Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid. Nayo timu ya Lyon imemwambia Wenger kutoa kima cha pauni milioni 60 ili kumchukua mshambulizi Alexandre lacazette. Haya yanajiri huku jarida la Independent likidai kuwa mpishi mkuu wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil anawazia kurudi timu yake ya zamani Real Madrid.