Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, NAIBU Mwalimu mkuu, Walimu watatu, Wanafunzi sita na mzazi wanaendelea kuzuiliwa na maafisa wa polisi kwa kipindi cha siku 10 kwa kuhusishwa na kuteketezwa kwa bweni la shule ya upili ya Karbanet.
Wanafunzi hao na mzazi walikamatwa na kufikishwa mahakamani walikokabiliwa na mashtaka ya uteketezaji kabla ya walimu hao watatu kukamatwa kufuatia maandamano ya wananfunzi na kisha kufunguliwa mashtaka sawa na hayo.
Kwingineko,
Washukiwa wawili akiwamo mwalimu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya St.Teresa’s Kaunti ya Trans-Nzoia wameshtakiwa kwa madai ya kupanga kuteketeza shule.
Hata hivyo, hawakuruhusiwa kukana au kubali mashtaka kwa msingi kuwa maafisa wa polisi walihitaji muda zaidi wa kuwachunguza kabla kuwafungulia mashataka.
Keep Reading
- Ways parents can help children set New Year resolutions
- How to parent purposefully this year
- Why structure is your child's greatest security
- Art of parenting highly sensitive children
Wakati uo huo, katika Kaunti ya Kisii ambayo imeathirika zaidi na visa vya uteketezaji wa majengo ya shule, Kamishna wa Kaunti hiyo Kula Hache amepiga marufuku uuzaji wa mafuta ya petroli kwa wanafunzi.