Omar Mohammed Omar amenaswa katik mtego wa dawa za kulevya kwa miaka 23 sasa mjini Mombasa. Hali iliyomdhoofisha kiasi cha kutelekezwa na familia na marafiki waliochoshwa na hali yake. Omar amejaribu kuwacha uraibu huu lakini wapi,huyu hapa Omar akielezea masaibu yake ambayo ni hadithi ya wengi wanaoishi mafichoni kwa hofu ya kejeli ya jamii.