Hatma ya naibu wa jaji mkuu nchini nancy baraza itajulikana siku ya ijumaa mwendo wa saa nane unusu. Akitangaza haya baada ya kikao na makamishna wa tume ya huduma za mahakama, jsc jaji mkuu nchini dakta willy mutunga alisema kwamba wamebuni kamati ndogo itakayochunguza tukio la madai ya utovu wa nidhamu ulioripotiwa. Wakati huohuo,chama cha wanasheria nchini kimewataka wakenya kuwa na subira,hasa wakati huu ambapo uchunguzi unaendelea kuambatana na kisa hicho. Ali manzu na taarifa zaidi