Kisa cha naibu jaji mkuu nancy baraza kimeibua historia ya jinsi vigogo serikalini huwa na mwenendo wa maringo kupita kiasi na kuwatweza wananchi pindi wanapokuwa katika maeneo ya umma. Na kwa wale wanaodhania wanaonewa sheria za maadili ya afisa wa umma zinawashinikiza kuheshimu watu katika shughuli rasmi na vile vile  wanapoendesha maisha yao kibinafsi. Huu utakuwa mtihani mkubwa kwa idara ya mahakama ikiwa watatekeleza haki kuambatana na sheria hiyo ya maadili. Baraza la tume ya mahakama litakutana jumatatu ijaayo kutafakari kisa hiki cha naibu jaji mkuu, baada ya jaji mkuu willy mutunga kuonya kuwa hakuna yeyote ambaye sheria itamlinda.