Watu waliojihami walivamia vijiji vya Laisamis huko Marsabit na kuiba ngamia wapatao mia mbili; mbuzi na kondoo ambao idadi yao inakisiwa kuwa elfu tano. Taharuki imetanda katika sehemu hiyo, hii ikiwa ni wiki chache tuu baada ya watu watatu kuuawa kwenye mashambulizi makali dhidi ya manyatta za Samburu na mifugo kadhaa kuibwa.