Watu wanne wamefariki na wengine 45 wanauguza majeraha ya moto siku kumi tu baada ya ule mkasa wa sinai. Maafa hayo yalitokea eneo la matayos, busia pale waathiriwa hao walipokuwa wakichota mafuta kutoka kwenye trela moja la kusafirisha mafuta lililokuwa likielekea uganda lilipopoteza mwelekeo. Inadaiwa kuwa trela hilo lilishika moto baada ya dereva wa trela wa hilo kujaribu kuchomoa nyaya zake za betri.