Mwenyekiti wa tume ya utekelezaji wa katiba abdikadir mohammed ametaja malumbano yanayoshuhudiwa baina ya afisi kuu za serikali zinazoshughulikia utekelezaji wa katiba kama kikwazo cha utekelezaji wa katiba mpya. .kufikia sasa takriban miswada 15 haijashughulikiwa kikamilifu licha ya kuwa yamesalia takriban majuma matatu kabla ya muda uliotengwa kukamilika.kutokana na hilo abdikar ameagiza waziri wa sheria, mkuu wa sheria na mwenyekiti wa tume ya utekelezaji wa katiba kufika mbele ya kamati hiyo siku ya alhamisi.