Siku chache kabla ya taifa jipya la Sudan kuanza rasmi kujitawala,waasi wamegeuka na kuwa tisho jipya kwa taifa ambalo limepigana kwa zaidi ya miaka 21. Taifa hilo limeathiriwa kiasi cha kwamba baadhi ya majimbo yametekwa nyara kabisa na waasi waliojitenga na jeshi la SPLA linalodaiwa kuwa jeshi linalotawaliwa katika misingi ya ukabila likisemekana kumilikiwa na kabila la dinka ,ambalo ni kabila la rais .changamoto kubwa iliopo sasa ni jinsi ya kupunguza idadi yao na kuhakikisha kwamba hatawatojiunga na waasi misituni.mwanahabari wetu Purity Mwambia ambaye alizuru nchini Sudan ametuandalia sehemu yetu ya pili ya makala ya mizingile ya utawala na kufichua sura za waasi Sudan


Sudan: Mizingile part 2