Rais kibaki na waziri mkuu raila odinga aidha hawawezi au hawataki kupambana na ufisadi nchini. Ndio msimamo wa waziri wa ardhi sally kosgey alipozungumza kwa kina na balozi wa marekani humu nchini michael rannerberger na maafisa wa ngazi ya juu wa marekani. Ufichuzi huu katika tovuti ya wikileaks pia unamnukuu kosgey wakati huo akiwa waziri wa elimu ya juu akisema ingawa aliamini raila odinga alikuwa na moyo wa mageuzi, kizingiti ni kuwa raila hataki kuwafuta kazi washirika wake waliohusishwa na ufisadi na kwamba anatawalwa sana na masuala ya itifaki badala swala nyeti la mageuzi kamili.