Waathiriwa wengi wa ghasia za baada ya uchaguzi ni wale wanaoishi katika mitaa ya mabanda. Kina mama walibakwa na kuwachwa bila waume na wanao,wasiweze kujipatia riziki baada ya hapo. Hata hivyo, wanawake na waume katika mtaa wa mabanda wa kibera wameamua kubadilisha hali yao ya kichumi kwa kufanya ukulima. Amini usiamini,katikati mwa mtaa huo, kuna mashamba ambayo yanazaa mazao kupita ilivyotarajiwa, huku wakitumia nafasi hiyo sio tuu kulisha jamii, bali kuzungumza kuhusu machungu waliyoyapitia na hapo kuponya nafsi zao. Esther Kahumbi anatuletea taarifa hiyo katika makala ya leo ya Maisha Peupe