Maafisa wa kijeshi mjini Eldoret wanadaiwa kuhusika na ufisadi baada ya kumchuja msichana mmoja kutoka Baringo hata baada ya kuajiriwa na serikali kama mwanajeshi kwa madai ya kuwa mja mzito. Ajabu ni kwamba madaktari watatu wa serikali wamedhibitisha kuwa msichana huyo si mja mzito, na hata maafisa katika kambi ya makurutu wa jeshi kukiri kweli dada huyo si mja mzito, hata hivyo dada huyo alipoomba kurejeshwa kambini aendelee na mafunzo, alielezwa nafasi yake kesha chukuliwa na kurutu mwingine na kumshauri ajaribu mwaka ujao.