Kuidhinishwa kwa katiba mpya sasa kunaonekana kuwatia wengi tumbo joto haswa viongozi wanaodaiwa kujihusisha na maswala ya ufisadi huku mkono mrefu wa sheria ukiwafuata unyo unyo. Sheria ambayo sasa imepelekea viongozi wetu kujikuta kizimbani hivi majuzi na hata wengine kukabiliwa na kamati za bunge kuhusu madai ya ufisadi kutoka wizara mbali mbali. Je sheria hizi mpya zinasema nini kuhusu maadili ya wafanyikazi wa umma?