Imedhibitishwa kuwa mtoto akinyonyeshwa kwa miezi sita mfulululizo baada ya kuzaliwa basi huweza kuepukana na magonjwa ambayo huwaandama watoto wachanga. Basi kina mama wanahimizwa kuhakikisha kuwa wanao wananyonya kikamilifu na waajiri kuwawezesha wafanyikazi wao wa kike kutekeleza shughuli hii kwa kuwapa mahala pa kufanyia hivyo ikiwa ni pamoja na kuwapa muda wa kutosha wa kuwanyonyesha wanao.